Submission

Submission — Ujisalimishaji (Uislamu): chanzo kikuu duniani cha habari sahihi kuhusu Uislamu wa kweli, katika lugha 33

Kurani 3:77 — Waamramu (Ali-'Imran)

Kuhusu wale wanaovunja agano la Mungu na majukumu yao kwa bei ya chini, hawatapata sehemu yoyote katika Akhera. Mungu hatawasemeza, wala kuwatizama, Siku ya Kiyama, wala hatawatakasa. Wamejiletea adhabu chungu.

[3:76] Hakika, wale wanaotimiza majukumu yao na kuishi maisha ya haki, MUNGU huwapenda wenye haki.

[3:78] Miongoni mwao wamo wale wanaopotosha ndimi zao kufanana na maandiko, ili upate kuamini kuwa ni kutoka kwenye maandiko, ilhali si kutoka kwenye maandiko, na wanadai kuwa ni kutoka kwa MUNGU, ilhali si kutoka kwa MUNGU. Hivyo, wanatoa uwongo na kuviweka kwa MUNGU, wakijua kufanya hivyo.