Kurani 48:25 — Ushindi (Al-Fatt-h)
Ni wao walio kufuru na kukuzuia kuingia Msikiti Mtakatifu, na hata kuzuia matoleo yako kufika mahali pake. Kulikuwepo na wanaume na wanawake waumini (katika kambi ya adui) ambao hukuwa hawajui, na ulikuwa karibu kuwadhuru bila kujua. Mwenyezi Mungu humpa rehema yake amtakaye. Wakikaidi, atamlipa wale miongoni mwao wanao kufuru kwa adhabu chungu.
[48:24] Yeye ndiye Aliyewazuia mikono yao isikudhuru, na akazuia mikono yako isiwadhuru wao katika bonde la Maka, baada ya kukupeni ushindi juu yao. Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuona kila unachotenda.
[48:26] Wakati wale ambao hawakuamini walikasirika, na mioyo yao ilijaa kiburi cha siku za ujinga, MUNGU aliwabariki mjumbe wake na waumini kwa utulivu na kuridhika, na kuwaongoza kushikilia neno la haki. Hii ndiyo walioistahili vema. MUNGU anajua kabisa mambo yote.