Sura 97: Bahati (Al-Qadr)
Kwa jina la Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.
[97:1] Tulifunua hayo katika Usiku wa Qadr.*
[97:2] Jinsi gani usiku wa Qadr ulivyo mzuri!
[97:3] Usiku wa Qadr ni bora kuliko miezi elfu.
[97:4] Malaika na Roho hushuka humo kwa idhini ya Mola wao, kutekeleza kila amri.
[97:5] Amani ipo hadi kufika kwa alfajiri.