Kurani 40:63 — Msamehevu (Ghafer)
Wanapotenga ni wale wanaopuuza maonyo ya MUNGU.
[40:62] Hivyo ndivyo MUNGU wako Mola, Muumba wa vitu vyote. Hapana mungu ila Yeye. Vipi unaweza kupotea njia?
[40:64] MUNGU ndiye aliyeifanya dunia iweze kukaliwa na nyinyi, na anga kuwa ni muundo imara, na Aliyekuumba nyinyi, na akakuumba vizuri. Yeye ndiye anayewapa riziki njema. Huyo ndiye MUNGU wenu Mola; MUNGU Mkuu, Mola wa ulimwengu.