Kurani 6:88 — Mifugo (Al-An'am)
Hivyo ndivyo mwongozo wa MUNGU ulivyo, ambao kwayo huwaongoza waja wake wale wamtakao. Kama yeyote wao angeangukia ibada ya sanamu, matendo yao yangelifutika.
[6:87] Miongoni mwa mababu zao, wazawa wao, na ndugu zao, tulichagua wengi, na tukawaongoza kwenye njia iliyonyooka.
[6:89] Hao ndio ambao tumewapa maandiko, hekima, na unabii. Ikiwa watu hawa watakataa, tutawabadilisha na wengine badala yao, na watu hao wapya hawatakuwa makafiri.