Kurani 10:35 — Yunus (Yunus)
Sema, "Je, mmoja wa sanamu zenu huongoza kwenye ukweli?" Sema, "MUNGU huongoza kwenye ukweli. Je, yule anayeongoza kwenye ukweli ni zaidi wa kufuatwa, au yule asiyeongoza na anahitaji uongozi kwa ajili yake mwenyewe? Kuna nini kibaya na hukumu yako?"
[10:34] Sema, "Je, kuna mmoja wa sanamu zenu anaweza kuanzisha uumbaji, kisha kuurudia?" Sema, "MUNGU ndiye anaye anzisha uumbaji, kisha kuurudia."
[10:36] Wengi wao wanafuata dhana tu, na dhana haiwezi kuchukua nafasi ya ukweli. MUNGU anajua kabisa kila wanachofanya.