Kurani 10:92 — Yunus (Yunus)
"Leo, tutahifadhi mwili wako, ili kukusimamisha kama somo kwa vizazi vijavyo."* Bahati mbaya, watu wengi hawana habari kabisa na ishara zetu.
[10:91] "Ni kuchelewa sana!* Kwa maana umekwisha kumuasi, na kuchagua kuwa mkosaji.
[10:93] Tumewapa Wana wa Israeli heshima kuu na kuwabariki na riziki nzuri. Hata hivyo, walizozana walipofikishiwa elimu hii. Mola wako atawahukumu Siku ya Kiyama kuhusu kila kitu walichozozana nacho.