Kurani 16:66 — Nyuki (Al-Nahl)
Na katika mifugo kuna mafunzo kwenu: tunakupeni kinywaji kutoka matumboni mwao. Kutoka katikati ya chakula kilichovunjwa na damu, mnapata maziwa safi, yenye ladha kwa wanywaji.
[16:65] MUNGU huteremsha kutoka mbinguni maji kufufua ardhi baada ya kufa. Hii inapaswa kuwa ithibati ya kutosha kwa watu wanaosikia.
[16:67] Na kwa matunda ya mikungu na zabibu mnazalisha vileo, pamoja na riziki nzuri. Hii inapaswa kuwa ithibati ya kutosha kwa watu wenye akili.