Kurani 2:225 — Ng'ombe (Al-Baqarah)
MUNGU hakuwajibishi kwa maneno matupu ya viapo; bali anakujibisha kwa nia zako za ndani. MUNGU ni Mwenye kusamehe, Mpole.
[2:224] Usiitweze jina la MUNGU kwa kula kiapo kwa kubahatisha, ili uonekane mwadilifu, mcha MUNGU, au kupata imani mbele ya watu. MUNGU ni Msikiaji, Mjuzi.
[2:226] Wale wanaotaka kuachana na wake zao wangoje miezi minne (kwa kupumzika); ikiwa wabadilisha maamuzi yao na kurejesha uhusiano, basi MUNGU ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.