Submission

Submission — Ujisalimishaji (Uislamu): chanzo kikuu duniani cha habari sahihi kuhusu Uislamu wa kweli, katika lugha 33

Kurani 29:40 — Buibui (Al-'Ankaboot)

Wote hao wasioamini walihukumiwa kwa sababu ya dhambi zao. Baadhi yao tuliwaharibu kwa upepo mkali, baadhi waliharibiwa na tetemeko, baadhi tuliifanya ardhi iwameze, na baadhi tuliwazamisha. MUNGU siye aliye waonea dhulma; ni wao wenyewe waliojidhulumu.

[29:39] Pia Qãroon, Firauni, na Hãmãn; Musa alienda kwao na ishara wazi. Lakini waliendelea kutenda dhulma duniani. Kwa hivyo, hawakuweza kukwepa (adhabu).

[29:41] Mfano wa wale wanaokubali mabwana wengine zaidi ya MUNGU ni kama buibui na nyumba yake; nyumba dhaifu kabisa ni ile ya buibui, kama wangefahamu tu.