Kurani 3:114 — Waamramu (Ali-'Imran)
Wanaamini MUNGU na Siku ya Mwisho, wanahimiza uadilifu na kukataza uovu, na wanaharakisha kutenda matendo mema. Hao ndio wenye haki.
[3:113] Hawako wote sawa; miongoni mwa wafuasi wa maandiko, kuna wale ambao ni wenye haki. Wanatafakari mafunuo ya MUNGU usiku kucha, na wanainama kusujudu.
[3:115] Mema yoyote wayafanyayo hayatakuwa bure. MUNGU anajua kabisa wenye haki.