Submission

Submission — Ujisalimishaji (Uislamu): chanzo kikuu duniani cha habari sahihi kuhusu Uislamu wa kweli, katika lugha 33

Kurani 3:156 — Waamramu (Ali-'Imran)

Enyi mlioamini, msifanane na wale ambao wamekufuru na wakasema kuhusu jamaa zao ambao walikwenda safarini au kujitayarisha kwa vita, "Wangelibaki nasi, wasingalikufa au kuuawa." Mwenyezi Mungu amewafanya hao kuwa na huzuni mioyoni mwao. Mwenyezi Mungu ndiye anayeamua kati ya uzima na kifo. Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuona kila mnayoyafanya.

[3:155] Hakika, wale miongoni mwenu waliogeuka siku majeshi mawili yalipokutana wamedanganywa na shetani. Hii inaonyesha baadhi ya matendo mabaya waliyoyafanya. MUNGU amewasamehe. MUNGU ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.

[3:157] Kama utauawa au kufa katika njia ya MUNGU, msamaha kutoka kwa MUNGU, na rehema ni bora zaidi kuliko chochote wanachojilundikia.