Submission

Submission — Ujisalimishaji (Uislamu): chanzo kikuu duniani cha habari sahihi kuhusu Uislamu wa kweli, katika lugha 33

Kurani 30:45 — Warumi (Al-Ruum)

Kwa kuwa atawalipa wale wanaoamini na kuishi maisha ya haki kutokana na neema zake kwa ukarimu. Hapendi wale wasioamini.

[30:44] Yeyote anaye kufuru, anakufuru kwa kudhuru nafsi yake mwenyewe, wakati wale wanaoishi maisha ya haki, wanafanya hivyo kwa lengo la kuimarisha na kukuza nafsi zao wenyewe.

[30:46] Miongoni mwa ishara zake ni kwamba Anapeleka pepo kwa dalili njema, ili kuwanyeshea rehema Zake, na kuruhusu meli ziende baharini kwa mujibu wa amri Zake, na ili muutafute utajiri wake (kupitia biashara), ili mpate kuwa wenye shukrani.