Submission

Submission — Ujisalimishaji (Uislamu): chanzo kikuu duniani cha habari sahihi kuhusu Uislamu wa kweli, katika lugha 33

Kurani 35:3 — Mwanzilishi (Faater)

Enyi watu, kumbukeni baraka za MUNGU juu yenu. Je, kuna muumba mwingine isipokuwa MUNGU ambaye hukustawisheni kutoka mbinguni na duniani? Hapana mungu mwingine ila Yeye. Vipi mnaweza kupotea njia?

[35:2] Wakati MUNGU anawabariki watu kwa rehema, hakuna nguvu inayoweza kuzuia. Na ikiwa Ataizuia, hakuna nguvu, isipokuwa Yeye, inayoweza kupeleka. Yeye ni Mwenye nguvu zote, Mwenye hikima zaidi.

[35:4] Ikiwa watapinga, mitume kabla yako walipingwa. MUNGU ana mamlaka juu ya vitu vyote.