Submission

Submission — Ujisalimishaji (Uislamu): chanzo kikuu duniani cha habari sahihi kuhusu Uislamu wa kweli, katika lugha 33

Kurani 5:73 — Karamu (Al-Ma'edah)

Wapagani kweli ni wale wanaosema kwamba MUNGU ni sehemu ya tatu ya Utatu. Hakuna mungu ila mungu mmoja. Isipokuwa wakae kimya wasiseme hivi, wale wanaokataa miongoni mwao watapatwa na adhabu chungu.

[5:72] Waabudu masanamu kweli ni wale wanaosema kwamba MUNGU ni Masihi, mwana wa Maryamu. Masihi mwenyewe alisema, "Enyi Wana wa Israeli, mmsujudieni MUNGU; Mola wangu na Mola wenu." Yeyote anayemweka sanamu yoyote badala ya MUNGU, MUNGU amemharamishia Pepo, na hatima yake ni Moto. Wenye dhambi hawana wa kuwasaidia.

[5:74] Je! Hawataki kutubu kwa Mungu, na kuomba msamaha wake? Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu sana.