Kurani 5:79 — Karamu (Al-Ma'edah)
Hawakukatazana kutenda maovu. Kile walichofanya ni cha kusikitisha sana.
[5:78] Wamehukumiwa wale waliokataa kuamini miongoni mwa Wana wa Israeli, kwa ulimi wa Daudi na Yesu, mwana wa Maryamu. Hii ni kwa sababu walipuuza na kuvuka mipaka.
[5:80] Utaona wengi wao wakiunga mkono wale wasioamini. Ni jambo la kusikitisha sana kwa vile mikono yao imetuma mbele kwa niaba ya nafsi zao. MUNGU amekasirika nao na hivyo watakaa milele katika adhabu.