Submission

Submission — Ujisalimishaji (Uislamu): chanzo kikuu duniani cha habari sahihi kuhusu Uislamu wa kweli, katika lugha 33

Kurani 57:18 — Chuma (Al-Hadeed)

Hakika, wanaume na wanawake wenye kutoa misaada wamemkopesha MUNGU mkopo wa wema. Watazipokea thawabu zao zilizozidishwa maradufu; wamestahili malipo mazuri sana.

[57:17] Jua kwamba MUNGU hufufua ardhi baada ya kufa kwake. Hivyo tunaeleza ishara kwa ajili yenu, ili mpate kuelewa.

[57:19] Wale waliomwamini MUNGU na wajumbe wake ni watakatifu na mashahidi. Wametengewa tuzo zao na mwanga wao kwa Mola wao. Kuhusu wale waliokataa na kukataa maonyo yetu, wamejipatia Moto.