Submission

Submission — Ujisalimishaji (Uislamu): chanzo kikuu duniani cha habari sahihi kuhusu Uislamu wa kweli, katika lugha 33

Kurani 6:149 — Mifugo (Al-An'am)

Mungu ana hoja yenye nguvu zaidi; akipenda, anaweza kuwaongoza nyote.

[6:148] Wanaoabudu sanamu husema, "Kama MUNGU angependa, tusingefanya ibada ya sanamu, wala wazazi wetu, wala tusingepiga marufuku chochote." Hivyo walivyofanya wale walio kuwa kabla yao kwa kukufuru, mpaka walipokumbana na adhabu yetu. Sema, "Je, mnayo elimu thabiti mnayoweza kutuonyesha? Mnafuata dhana tu; mnafanya makadirio tu."

[6:150] Sema, "Leteni mashahidi wenu watakao shuhudia kwamba MUNGU ame kataza hili au lile." Wakishuhudia, usishuhudie nao. Wala usifuatishe maoni ya wale wanaokataa ishara zetu, na wale wasioamini Akhera, na wale wanaopotea njia kutoka kwa Mola wao.