Kurani 2:13 — Ng'ombe (Al-Baqarah)
Wakiambiwa, "Aminini kama walivyo amini watu wengine," husema, "Je, tutamini kama wapumbavu walivyo amini?" Kwa hakika, wao ndio wapumbavu, lakini hawajui.
[2:12] Kwa kweli, wao ni watenda maovu, lakini hawatambui.
[2:14] Wawapo na waumini husema, "Tunaamini," lakini wakiwa peke yao na mashetani yao husema, "Tuko pamoja nanyi; tulikuwa tunacheza tu."