Kurani 4:100 — Wanawake (Al-Nesa')
Yeyote anaye hamia katika njia ya MUNGU atapata baraka kubwa na utajiri duniani. Yeyote anayeacha nyumba yake, kuhama kwa MUNGU na Mtume wake, kisha kifo kinamfikia, malipo yake yamehifadhiwa na MUNGU. MUNGU ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
[4:99] Haya yanaweza kusamehewa na MUNGU. MUNGU ni Mwepesi wa Kusamehe, Mwenye Kusamehe.
[4:101] Unapokuwa safarini wakati wa vita, hufanyi kosa lolote kwa kupunguza Sala zako, ikiwa unahofia kuwa makafiri wanaweza kukushambulia. Hakika, makafiri ni maadui wenu wenye bidii.