Submission

Submission — Ujisalimishaji (Uislamu): chanzo kikuu duniani cha habari sahihi kuhusu Uislamu wa kweli, katika lugha 33

Kurani 3:177 — Waamramu (Ali-'Imran)

Wale wanaochagua kukataa imani badala ya kuamini, hawamuumizi MUNGU hata kidogo; wamejiletea adhabu chungu.

[3:176] Usiwe na huzuni kwa wale wanaoharakisha kukataa imani. Hawamuumizi MUNGU hata kidogo. Badala yake, MUNGU ameona watakuwa hawana sehemu yoyote Akhera. Wamejiletea adhabu kali.

[3:178] Wacha wasioamini wasidhani kwamba tunawaongoza kwa manufaa yao wenyewe. Tunawaongoza ili kuthibitisha uovu wao tu. Wamejiletea adhabu ya kudhalilisha.